Windows

HESABU ZA COASTAL UNION ZAHAMISHIWA HUKU


KOCHA wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema kwa sasa hesabu zake ni kuona anapata matokeo kwenye mchezo wake unaofuata dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Machi 9 Uwanja wa Kaitaba.

Coastal Union haijawa na matokeo chanya kwenye mechi zake mbili mfululizo za ugenini ambapo ilipoteza mbele ya Mtibwa Sugar kabla ya kupoteza mbele ya JKT Tanzania.

Mguda amesema kuwa matokeo wanayopata ni kipindi cha mpito, wakati unakuja ambao watakuwa na furaha kama awali.

"Kwa sasa matokeo tunayopata ni mapito, wakati wetu unakuja na maandalizi yetu ni makubwa kuelekea mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar, kikubwa sapoti kutoka kwa mashabiki," amesema Mgunda.

Coastal Union wanashika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo 28 wakiwa na pointi 34.


Post a Comment

0 Comments