KUTOKA KATIKA KURASA ZA MITANDAO YA KIJAMII ZA YANGA WAMEANDIKA
MREJESHO RASMI WA KAMATI MAALUMU YA YANGA UTAANZA KULETWA LEO 20/03/2019 KWA AWAMU*
Kuanzia leo Kamati Maalumu itakuwa inaleta kwa Awamu Mrejesho wa Mpango Mkakati uliozingatia *HADIDU ZA REJEA* kwa wanachama na Wapenzi wa Yanga ili kujenga uelewa Thabiti miongoni mwao ili kufikia Malengo Kusudiwa.
Wanachama na Wapenzi wote wa Klabu ya Yanga wanatambua kuwa kwasasa tunakabiliwa na changamoto kadhaa ikihusisha suala la ukosekanaji wa vyanzo vya uhakika vya mapato kwa muda mrefu sasa.
Kwasababu hiyo Klabu ya Yanga kwa kushirikiana na Wadau Mbalimbali chini ya Uratibu wa Kocha Mwinyi Zahera walibuni njia bora na endelevu ya kuweza kupata pesa kwa haraka na kuweka mfumo bora wa kuendeleza kitakachopatikana.
Kupitia ushirikiano huo ambao uliratibiwa vyema na Wachezaji pamoja na Benchi la Ufundi walifungua Akaunti ya Kukusanyia fedha *YANGA COLLECTION A/C No: 0150419775800 CRDB BANK – VIJANA BRANCH* ili wapenzi na wanachama wa Yanga waweze kuchangia timu yao. 
Katika kuboresha wazo hili zuri na jema Uongozi wa Yanga uliunda Kamati Maalumu ya Kuhamasisha Uchangiaji *09/03/2019* ili ibuni na kuweka Mikakati madhubuti kufanikisha zoezi hili ndani ya muda mchache ili Klabu ya *YANGA* iweze kujikwamua kiuchumi. 
Kamati hiyo ilipewa *HADIDU TANO ZA REJEA* kama ifuatavyo;
i) Kuandaa Mpango Kazi wa kufanikisha zoezi hili la uchangiaji kwenye Klabu ya Yanga kwa muda mfupi, Kati na Mrefu.
ii) Kuandaa Mkakati maalumu wa namna nzuri ya kukusanya pesa kwa watu ambao wana mapenzi na Yanga bila kujali rika, jinsia na maumbile yao.
iii) Kuboresha Mkakati uliopo sasa wa ukusanyaji pesa pamoja na kuandaa mpango wa utunzaji wa pesa zitakazo kusanywa pamoja na mrejesho kwa wachangiaji.
iv) Kuzindua rasmi mpango wa uchangiaji ili uweze kuleta tija na kufikia malengo yaliyokusudiwa.
v) Kuushauri uongozi wa Yanga juu ya njia sahihi na bora zaidi kwa siku za usoni ili kuwa na Yanga imara.