Windows

BODI YA LIGI YAIBUKA NA KUZUNGUMZIA SAKATA LA ARUSHA UNITED KUJITOA DARAJA LA KWANZA


Mkurungenzi wa Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, amesema kuwa maamuzi ya malalamiko kutoka kwa vilabu hutolewa baada ya kamati husika kutolewa.

Akizungumza na Radio One, Wambura amesema tatizo lolote linalopita klabu na wakipokea malalamiko, kamati husika hukaa na kujadili kisha kuja na maamuzi stahiki.

Kauli ya Wambura imekuja kutokana na timu inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, Arusha United kutangaza kujiondoa katika ligi hiyo kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wake.

Kwa mujibu wa uongozi wa Arusha United, umesema ligi imekuwa ikienda ilimradi bila hatua zozote kuchukuliwa na TFF ambao ndiyo mama wa soka la nchi.

Arusha imejitoa kwenye ligi hiyo wakisema wamekuwa wakituma malalamiko yao sehemu husika ambayo ni TFF lakini hakuna hatua zozote ambazo zimekuwa zikichukuliwa.

Post a Comment

0 Comments