

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera ameendelea kusisitiza kuwa kamwe hatohitaji kurejeshewa pesa zake ambazo anaisaidia timu hiyo.
Kauli ya Zahera imekuja baada ya kuwepo kwa minong'ono kutoka kwa baadhi ya wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuwa ataanza kuidadi hapo baadaye.
Zahera ambaye yupo jijini Mwanza na kikosi cha Yanga kwa mechi ya ligi dhidi ya Mbao FC leo jioni, ameeleza kuwa ataendelea kujitolea kuisaidia timu ambayo inapitia wakati mgumu hivi sasa.
"Sitohitaji malipo yoyote baadaye kutoka Yanga, nimeamua kujitoa kuisaidia timu kutokana na hali ngumu inayopitia hivi sasa, nina kazi zangu zingine zinazoniingizia hela na sitegemei Yanga pekee" alisema.
Aidha, Zahera amewataka wanachama na mashabiki wa Yanga kuendelea kuichangia klabu yao kwa nguvu zote ili kuisaidia kuweka morali katika mechi zijazo za ligi.




0 Comments