Windows

YANGA WAPANIA KULIPA KISASI BAADA YA KICHAPO KWA MNYAMA, WATAJA KILICHOWABEBA WAPINZANI WAO




MWINYI Zahera amesema kuwa kisasi chake dhidi ya Simba bado kipo anaanza maandalizi sasa ili kuwanyoosha katika msimu ujao endapo watakutana kwenye Ligi Kuu Bara.

Mbinu za Zahera zilizidiwa na mbelgiji wa Simba Patrick Aussems kwenye mchezo wao wa marudio dakika ya 71 Uwanja wa Mkapa baada ya wachezaji wake kufanya makosa yaliyoigharimu timu yake na kuruhusu kufungwa bao 1-0.

"Nimefungwa ni kweli sikuwa na namna maana wachezaji wangu mbinu walizidiwa ila kama ambavyo mnaona hakuna namna nyingine yoyote ya kukifananisha kikosi changu na wapinzani wangu.

"Nawaambia wazi kama ambavyo nimekuwa nikiwaambia, mwakani hawa watanitambua nina amini nitalipiza kisasi hiki kwani kwa sasa wachezaji nilionao wengi asilimia kubwa sio wale ambao niliwachagua mimi," amesema.

Yanga wamepoteza michezo miwili kati ya 23 waliyocheza kwa sasa ambapo walianza kupoteza mbele ya Stand United na mchezo wao wa pili ni dhidi ya Simba.

Post a Comment

0 Comments