Aliye kuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura, amesema atarudi mahakamani kufungua kesi ya madai kuishtaki TFF kwa kukaidi maamuzi yaliotolewa na Mahakama ya kumrejesha madarakani katika shirikisho hilo
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es salaam, Wambura amesema rais wa TFF amekaidi maamuzi ya mahakama, kitendo alichokieleza kuwa ni kudharau mamlaka ya muhimili huo ambao ni chombo pekee kinachotoa maamuzi ya mwisho kisheria
Hata hivyo wambura amesema aliandika barua kwenda Shirikisho la soka Duniani FIFA na tayari ameshapokea majibu kutoka kwa katibu mkuu wa shirikisho hilo.
Wambura amefungiwa maisha na FIFA kujihusisha na soka akituhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo uhujumu uchumi,na ubadhilifu wa Mali za shirikisho, makosa amabayo amekana na kwenda mahakamani kupinga kuondolewa kwa wadhifa wake.
0 Comments