KIKOSI cha Simba leo kimetia timu jijini Arusha baada ya kuondoka asubuhi kwa ndege kupitia Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Simba wamepokelewa kishujaa na mashabiki wa Arusha baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Meddie Kagere dhidi ya watani wao Yanga mchezo uliochezwa jana uwanja wa Taifa.
Simba hawakutaka kupumzika leo kwani walianza mazoezi jioni kwa ajili ya kurejesha miili sawa.
Simba watakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya African Lyon utakaochezwa Jumanne ya Februari 19, Uwanja Amri Abeid.
0 Comments