Windows

MWINYI ZAHERA ALIVYOZUNGUMZIA TAARIFA ZA KUCHUKUA NAFASI YA PLUJIM




MWINYI Zahera, kocha mkuu wa Yanga amesema hana taarifa za kuajiliwa na uongozi wa Azam FC kuchukua nafasi ya mholanzi Hans Pluijm ambaye ametimuliwa na msaidizi wake Juma Mwambusi.

Uongozi wa Azam FC umefikia hatua hiyo ya kumtimua Pluijm kutokana na mwenendo mbovu wa matokeo kwenye ligi baada ya hivi kwa kuanza na Alliance FC (1-1), Lipuli (1-1), Prisons (1-0), Coastal Union (1-1) na Simba (3-1).

Zahera amesema bado yupo Yanga kwa sasa hivyo mashabiki wasiwe na mashaka endapo kutakuwa na mabadiliko ataweka kila kitu wazi.

"Mpaka sasa sijapigiwa simu na viongozi wa Azam FC kuzungumza nao pia sijaonana na viongozi wa Azam FC na hakuna chochote ambacho kinaendelea kwa sasa.

"Siwajui viongozi wa Azam FC kwa kuwa sijawahi kuonana nao zaidi ya wao kuniona nikiwa kwenye vyombo vya habari ama kukutana tukiwa kazini suala la kukaa nao bado sijalifanya," amesema Zahera.

Uongozi wa Azam FC umesema kuwa tayari tangu jana walianza mchakato wa kumtafuta kocha mpya na kwa sasa timu ipo chini ya kocha Iddy Cheche.

Post a Comment

0 Comments