PATRICK Aussems, kocha mkuu wa Simba raia wa Ubelgiji atakutana na Azam FC iliyo chini ya Mholanzi Hans Pluijm huku rekodi zikionekana kumbeba Mbelgiji huyu mbele ya wapinzani hao katika michezo yao ya hivi karibuni.
Mpaka sasa Simba ikiwa chini ya Aussems kwenye michezo mitatu ya Ligi Kuu Bara imebeba pointi zote tisa na kufunga jumla ya mabao saba katika michezo hiyo.
Kwa matokeo hayo yanaipoteza Azam FC ambayo imecheza michezo yake minne na kujikusanyia pointi tatu pekee na kufunga jumla ya mabao matatu.
Michezo ambayo Mbelgiji aliiongoza Simba ya ligi ni dhidi ya Mwadui FC ambapo ilishinda kwa mabao 3-0, Yanga ambapo ilishinda bao 1-0 na African Lyon ilishinda mabao 3-0.
Mholanzi aliongoza Azam dhidi ya Alliance alilazimisha sare ya kufungana bao 1-1, Lipuli sare ya bao 1-1, Tanzania Prisons alifungwa bao 1-0 na ule dhidi ya Coastal Union sare ya bao 1-1.
Simba imecheza michezo 17 inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 42 huku Azam FC wakiwa nafasi ya pili wamecheza michezo 24 wana pointi 50.
Ubabe wao utaendela kesho Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara,
0 Comments