Windows

KOCHA KMC: SIMBA NA YANGA WASAHU UBINGWA


Kocha mkuu wa timu ya Manispaa ya kinondoni Maarufu kwa jina la KMC amesema nia yake ni kutwaa taji la ligi kuu Tanzania bara akiwa na timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu.

Akizungumza na Global Tv baada ya mazoezi ya timu hiyo kujiandaa na mchezo dhidi ya mtibwa sugar kocha Ettiene Ndairajige ametamka kuwa nia yake ni kutwaa taji hilo licha ya timu yake kuwa katika nafasi ya tano mpaka sasa katika msimamo wa ligi hiyo

KMC imekuwa ikitajwa kuwa miongoni mwa timu zinazocheza kandanda safi miongoni mwa timu za ligi kuu Tanzania bara na wapo katika nafasi ya tano wakiwa na alama 37 zaidi ya alama 20 nyuma ya vinara wa ligi hiyo amabo ni yanga wenye alama 58.


Post a Comment

0 Comments