

Mwenyekiti wa Kamati ya Saidia Taifa Stars Ishinde Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo amekutana na wajumbe wa Kamati hiyo katika Kikao cha Kwanza kilichofanyika kwenye Hoteli ya Serena,Dar es salaam.
Kikao hicho kimefanyika ikiwa ni mkakati maalum wa kuanza kwa mipango ya kuiwezesha Taifa Stars kuibuka na ushindi dhidi ya Uganda katika mchezo ujao wa kuwania fainali za AFCON mwaka huu.
Stars itakuwa inakabiliwa na kibarua kigumu tarehe 22 Machi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Uganda, timu hizo mbili zilienda suluhu ya bila kufungana.




0 Comments