Windows

KAGERE AITEGA VIBAYA SIMBA


Mshambuliaji wa timu hiyo, Meddie Kagere ameitega klabu hiyo kutokana na suala la mkataba wake.

Hali hiyo inatokana na uwepo wa timu nyingi zilizo vizuri kiuchumi, kujitokeza kwa wingi kuhitaji kumsajili.

Wakala wa Kagere, Patrick Gakumba ameliambia Championi Ijumaa kuwa uongozi wa Simba unatakiwa kujipanga kama unataka kuendelea na mchezaji huyo kwa misimu mingine mara tu atakapomaliza mkataba msimu ujao. Alisema thamani ya mchezaji huyo kwa sasa imepanda na si kama ile ambayo Simba walimsajili wakati akitokea Gor Mahia ya Kenya.

Licha Gakumba kugoma kutaja dau la usajili ambalo Kagere alipewa na Simba lakini inadaiwa kuwa nyota huyo alipewa dola 60,000 (Sh 139m) na mshahara wa dola 5,500 kwa mwezi (Sh 12m).

“Dau la usajili ambalo Kagere alipewa na Simba siwezi kusema, hiyo ni siri ya ofisi lakini kwa sasa thamani yake imepanda ndiyo maana unaona timu mbalimbali zimekuwa zikitangaza madau makubwa ili kuhakikisha zinampata.

“Viongozi wa Simba wanatakiwa kujipanga kama watapenda kuendelea na Kagere mara tu mkataba wake utakapomalizika, kwa sasa bado ana mkataba wa mwaka mmoja kama na nusu hivi.

“Thamani yake kwa sasa ni kuanzia dola 300,000 (zaidi ya Sh 638m) hiyo ni kutokana na dau ambalo baadhi ya timu kadhaa za Afrika zimekuwa zikimtangazia ili zimsajili.

“Hivi karibuni TP Mazembe ilitangaza kutaka kumsajili lakini ikashindikana kutokana na mkataba wake na Simba, timu nyingine ni Raja Casablanca ya Morocco ambao walikuwa tayari kutoa dola 400,000 na mshahara wa dola 15,000 (Sh 34m) kwa mwezi, nilipowaambia viongozi wa Simba hawakuwa tayari kumwachia,” alisema Gakumba.

Post a Comment

0 Comments