Guaido, alitoa tangazo hilo katika maandamano yanayoendelea dhidi ya serikali mji mkuu wa nchi hio Caracas.
Spika huyo alisema, anakula kiapo cha kuwa rais wa muda wa Venezuela, kuunda serikali ya muda, kuandaa uchaguzi huru na wa haki na kumaliza manyanyaso ya serikali iliyopo.
Guaido alitolea wito umma umuunge mkono katika kazi hiyo kwa kusema wanajua kwamba hio sio kazi ya mtu mmoja, lakini matokeo yatapatikana, aliongeza kwamba hatoruhusu nguvu na matumaini ya nchi yao yapotee.
Guaido alisema maandamano hayo ya kuipinga serikali yataendelea kwa kusema kwamba hawatachoka mpaka pale watapoifikia tena demokrasia, uhuru, na pale maji na gesi asilia vitaporejea kwenye meza zao.Hawatachoka mpaka pale katika kila meza ya mvenezula mkate utapopatikana.
0 Comments