Na. Rahel Nyabali, Tabora.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega Amesema kuna umuhumu wa kufufua miundombinu ya kupakia na kushusha Ng'ombe Kupitia Usafiri Wa Treni Ya Mizigo Hatua Ambayo Itasaidia Kupunguza Adha Kubwa Ya Usafishaji Mifugo Wanayokumbananayo Wafanyabiashara Ya Ng’ombe.
Ameyasema hayo Wakati Alipotembelea Kituo Cha Usafishaji Cha Reli Ya Kati Mjini Tabora kwa kufanya mazungumzo ya kina na Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano kuhusu ili kuweza kurahisisha usafrishaji wa mifugo wanaotoka katika mnada wa Ipuli
Ulega amesema hakuna haja ya kubishana na wafugaji kwa sababu kunahaki ya wanyama na kuwa anahaki ndani ya masaa manane awe amekula na haki za mifugo na wanyama zinatakiwa zilindwe sio kwa Tabora hata kwa nchi nzima.
“Mimi nitazungumza na waziri Isaack kwamwerwe na mkulugenzi mkuu wa TRL Mh Kadogosa ili waweze kuona kunaumuhimu wa kufanya kazi kwa haraka sana ili tuweze kuwanusulu hawa wafugaji wetu na kulinda makubaliano yetu ," Amesema Ulega.
Hata hivyo, Miundombinu Katika Kituo Cha Usafirishaji Cha Reli Ya Kati Mjini Tabora Inaonekana Kusahaulika na kuwafanya wafanya biashara wa mifugo mkoani Tabora na maeneo ya jirani kufanya biashara hiyo katika mazingira magumu.
Aidh Naibu Waziri Ulega amewasihi Wafanyabiashara Wanaotumia Mnada Wa Ipuli Mjini Tabora Kufuata Na Kuzingatia Sheri, Kanuni Na Taratibu Ili Kuepuka Migongano Isiyokua Ya Lazima.
0 Comments