Windows

Matokeo ya Kidato cha nne yatangazwa, Wanafunzi 57 wafutiwa matokeo


Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limefuta matokeo ya wanafunzi 57 wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Tumaini Lutheran Seminari ya Malinyi mkoani Morogoro baada ya kubaini Shule hiyo kuvujisha mtihani huo.

Hayo yamesemwa  leo Alhamisi na Katibu Mkuu mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde wakati akitangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018 mkoani Dodoma.

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) leo  wametangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018 ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 1.29 kutoka asilimia 77.09 mwaka 2017 hadi asilimia 78.38.

Mbali na kufuta matokeo hayo, Necta imekifungia kituo hicho cha kufanyia mtihani, Amesema wameagiza wahusika wote kuchukuliwa hatua wakiwemo polisi waliosimamia, Dk Msonde ameanza kutangaza matokeo hayo leo saa 5:00 asubuhi.




Post a Comment

0 Comments