MABINGWA watetezi wa kombe la Ligi ya Wanawake Tanzania maarufu kama Serengeti Lite Women's Premier League wamepania kuwanyoosha Yanga Princess katika mchezo wao wa leo utakaochezwa Uwanja wa Mej.Gen.Isamuhyo.
JKT Queens hawajapoteza mchezo kati ya sita waliyocheza waliwanyoosha kwa bao 1-0 wapinzani wao wakubwa Simba Queens katika mchezo wao waliocheza Uwanja wa Karume hivi karibuni.
Kocha wa JKT Queens, Ally Ally amesema wanatambua ubora wa wapinzani wao hasa linapokuja suala la ushindani ila hesabu zao ni kumyoosha kila ajaye mbele yao kwa sasa.
"Sisi ni mabingwa watetezi na kazi yetu ni kuona tunatetea ubingwa wetu na ili tufanikiwe ni lazima tushinde michezo yetu yote ili tufikie malengo yetu.
"Kila mchezo una mipango yake mimi nikiwa ni mwalimu mbinu nilizotumia kuwafunga Simba zitakuwa tofauti na nitakazotumia leo kupambana na Yanga tutakapokuwa tunacheza Uwanjani," alisema Ally.
0 Comments