Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula ameshangazwa na halmashauri za wilaya ya Mpwapwa na Kongwa mkoani Dodoma kushindwa kuwafikisha katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi pamoja na baadhi yao kupelekewa ilani za madai.
Dk Mabula ameziagiza halmashauri hizo mbili kuhakikisha zinawafikisha wadaiwa hao katika Mabaraza ya Ardhi kwa hatua zaidi ambapo alielezea kuwa huko maamuzi yake ni mawili ambapo mdaiwa anatakiwa kulipa ama kunyanganywa miliki yake kufidia deni.
Naibu Waziri huyo alitoa agizo hilo jana alipozitembelea wilaya hizo mbili ikiwa ni mfululilzo wa ziara zake kutembelea halmashauri mbalimbali kwa nia ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi.
Kwa mujibu wa Dkt Mabula, halmashauri hizo zina wamiliki wengi wa viwanja wasiolipia kodi ya ardhi na hivyo kuzifanya kudai kiasi kikubwa cha fedha lakini idara za ardhi zinashindwa kuwachukulia hatua jambo linaloikosesha serikali mapapto.
Naibu Waziri wa Ardhi alisema, halmashauri ya wilaya ya Kongwa inadai jumla ya shilingi milioni 152 kutoka kwa wamiliki wasiolipa kodi huku ile ya Mpwapwa ikidai milioni 128,013,696.90.
0 Comments