MKALI wa ndondi, Francis Cheka, amefunguka kuwa kipigo alichopewa na Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ hakijamkatisha tamaa, anajipanga tena ili kuweza kulipa kisasi na kurudisha heshima yake.
Cheka alipigwa na Mbabe kwenye pambano la kufungia mwaka 2018 kwa ‘Technical Knock Out’ ya raundi ya sita na kupoteza ubingwa wa Dunia wa WBF kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba.
Cheka amesema kuwa hakuna bingwa atakayedumu milele na kwamba amekubali alizidiwa na Mbabe ila bado hajakata tamaa, anajipanga kurudi tena ulingoni ili kurudisha heshima yake.
“Hakuna bingwa atakayedumu milele, nakubali kuwa nilizidiwa ujanja na Dullah na akanipiga ila hilo haliwezi kunikatisha tamaa, najipanga kurudi ulingoni ili kurudisha heshima yangu,” alisema Cheka.
0 Comments